1 Corinthians 1:27-31

27 aLakini Mungu alivichagua vitu vipumbavu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye hekima, Mungu alivichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye nguvu. 28 bAlivichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa vya dunia hii, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko, 29 cili mtu yeyote asijisifu mbele zake. 30 dBali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Al-Masihi Isa, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu, yaani haki, na utakatifu na ukombozi. 31 eHivyo, kama ilivyoandikwa: “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana.”
Copyright information for SwhKC